Jeremiah 46:14-19


14 a“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,
hubiri pia katika Memfisi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
na Tahpanhesi:
Ni mji katika Misri.

‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,
kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’

15 dKwa nini mashujaa wako wamesombwa
na kupelekwa mbali?
Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana
atawasukuma awaangushe chini.

16 eWatajikwaa mara kwa mara,
wataangukiana wao kwa wao.
Watasema, ‘Amka, turudi
kwa watu wetu na nchi yetu,
mbali na upanga wa mtesi.’

17 fHuko watatangaza,
‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,
amekosa wasaa wake.’


18 g“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,
ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,
kama Karmeli kando ya bahari.

19 hFunga mizigo yako kwenda uhamishoni,
wewe ukaaye Misri,
kwa kuwa Memfisi utaangamizwa
na kuwa magofu pasipo mkazi.

Copyright information for SwhKC